Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu 119 cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 amefanya uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Katiak uteuzi huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu Msaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mweyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Aidha amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar:
1. Bwana Mabruki Jabu Makame
2. Bwana Feteh Saad Mgeni
3. Bwana Makame Juma Pandu
4. Dkt. Kombo Khamis Hassan
5. Jaji Khamis Ramadhan Abdulla
6. Bibi Jokha Khamis Makame
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 20 Juni 2018.
Wajume wote wa Tume ya Uchaguzi waliotajwa wanatakiwa kufika Ikulu siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2018 saa 4 za Asubuhi tayari kwa kuapishwa.