RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilieleza kwamba Rais Dk. Hussein Mwinyi amemteua Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 39 (1) na 39 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kabla ya Uteuzi huo Hemed Suleiman Abdulla alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 08 Novemba, 2020.

  • Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla  aliyeteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla aliyeteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.