Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakusudia kutoa Kibali cha Ajira Mpya katika Mwaka Mpya wa Fedha katika sekta ya Afya na Kada nyengine ili kukabiliana na Tatizo la Uhaba wa Wauguzi hapa Nchini
Rais Dķt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 12 Mei 2026 katika Kongamno kwanza la Kisayansi la Wauguzi lilioambatana na Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani, hafla iliofanyika Hoteli Verde ,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amewataka Wauguzi licha ya Tatizo la Uhaba wa Wauguzi kuwa Wastahamilivu na kutokata Tamaa pamoja na kuendelea kufanya kazi kwa Moyo na Weledi na kuzingatia Misingi ya kada hiyo muhimu katika sekta ya Afya.
Rais Dķt, Mwinyi amepongeza Mafanikio yaliopatikana Kitaaluma katika Miaka 62 ya Mapinduzi kutoka Wauguzi wa kawada kwa ngazi ya Stashahada hadi ngazi ya Uzamivu, Amesema mchango wa Wauguzi unazidi kuwa na thamani zaidi kutokana na Mabadiliko yaTeknolojia na Changamotio mpya za Kiafya.
Amelielezea Kongamano hilo la Kisayansi kuwa ni fursa na jukwaa muhimu la kujifunza mbinu mpya za Kitaalamu na kuimarisha Tafiti zitakazochangia huduma bora za Afya.
Rais Dķt, Mwinyi amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya itakabiliana na Changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika sekta ya Afya hususani Upungufu wa Wauguzi na Madaktari hapa Nchini pamoja na kuwaomba Washirika wa Maendeleo kushirikiana na Serikali kukabiliana na Changamoto za Kiafya na kuimarisha Rasilimali na Nguvu kazi kwa Mafunzo na Uimarishaji wa Miundombinu ya sekta ya Afya ikwemo Ujenzi wa Hosptali na Upatikanaji wa Vifaa.
Amefahamisha kuwa Wakati Serikali inajenga Hosptali Mpya za Mnazimmoja na Hospitali ya Saratani Binguni pia itahakikisha Ujenzi huo unaenda Sambamba na uletaji wa Vifaa vya kisasa ili kukidhi Mahitaji ya Hospitali za kisasa.
Akizungumza suala la Mafunzo kwa Wauguzi Amesema Serikali italifanyia kazi suala hilo ili kuwa na Sera nzuri ya Mafunzo itakayohakikisha inatoa Mafunzo kwa kila kada katika sekta ya Afya kwa kuwa na Utaratibu bora kwa Watendaji kujifunza.
Akihitimisha Hotuba yake Raiis Dkt Mwinyi amewahimiza Wauguzi kufanya kazi kwa moyo na huruma na kutoa huduma bora kwa Wagonjwa bila ya Ubaguzi, kuwa na Kauli nzuri, Ucheshi na kuzingatia Maadili ya Kada hiyo..
Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Mwaka ya 2026 yameadhimishwa Chini ya kauli Mbiu inayosema Kuwawezesha Wauguzi ni Kuokoa Maisha ( Empowerment Nurses,Saving lives)
