1. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Baraza la Michezo Namba 5 ya 2010, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Gulam Abdulla Rashid kuwa MWENYEKITI WA BARAZA LA MICHEZO, ZANZIABR. 

2. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 7(2) cha Sheria ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Namba 3 ya mwaka 2009, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Meja Jeneral Mstaafu Said S. Omar kuwa MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI. 

3. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya KMKM Namba 1 ya 2003, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Kapteni Khamis Simba Khamis kuwa NAIBU MKUU WA KIKOSI MAALUM CHA KUZUIA MAGENDO (KMKM).

4. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 12(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Namba 3 ya 2015, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Ndugu Farhat Ali Mbarouk kuwa MKURUGENZI WA IDARA YA MAZINGIRA katika Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira.

5. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Shirika la Nyumba Namba 6 ya 2014, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Ndugu Riziki Jecha Salim kuwa MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NYUMBA katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji.

6. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 15(1) cha Sheria ya Tawala za Mikoa Namba 8 ya 2014, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Ndugu Mkufu Faki Ali kuwa KATIBU TAWALA WA WILAYA YA WETE, PEMBA katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 17 Oktoba, 2017.