1. Bibi Hamida Ahmed Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara ya Zanzibar katika Wizara ya Biashara na Viwanda.

2. Bwana Omar Ramadhan Mapuri ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia, Zanzibar.

3. Bibi Mwanamkaa Abdulrahaman Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.

4. Dr. Abdul-Nasser Hamed Hikmany ameteuliwa kuwa Mrajis wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati,

5. Bwana Salum Kitwana Sururu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makumbusho na Mambo ya Kale katika Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 14 Juni, 2018.