Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameshiriki mazishi ya Marehemu Bi Safia Abeid,mama mzazi wa Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal yaliyofanyika huko kijijini kwao Kiboje Mwembeshauri, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa, dini na Serikali, wananchi pamoja na wanafamilia walihudhuria katika mazishi hayo ambapo mapema Alhaj Dk. Mwinyi aliungana nao katika sala ya kumuombea Marehemu iliyosaliwa huko Masjid Jaameh Zinjbaar, Mazizini, Jijini Zanzibar.