State House Blog

UZINDUZI WA TAWI LA BENKI YA CRDB MICHENZANI NA HUDUMA ZA ISLAMIC BANKING

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB na huduma za Islamic Banking Michenzani Mall katika Ukumbi wa Jengo la Michenzani Mall jijini Unguja (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Benk Bw.Al-Majid Mussa Nsekela akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CRDB Benki Bw Ally Laay.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB na huduma za Islamic Banking Michenzani Mall katika Ukumbi wa Jengo la Michenzani Mall jijini Unguja.
  • Baadhi ya waalikwa waliohudhuria katika hafla ya Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB na huduma za Islamic Banking Michenzani Mall,wakimsikiliza mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake katika Ukumbi wa Jengo la Michenzani Mall jijini Unguja
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akipokea cheti cha kupongezi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Benk Bw.Al-Majid Mussa Nsekela (kulia)kwa kutimiza mwaka mmoja wa Uongozi wake wakati alipowasili katika Ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB na huduma za Islamic Banking Michenzani Mall (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe Jamal Kassim Ali na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Benki Bw Ally Laay
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akipokea picha inayosomeka Uzinduzi wa Tawi la Benki ya CRDB Michenzani na huduma za Islamic Banking zimezinduliwa rasmi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Benk Bw.Al-Majid Mussa Nsekela hafla iliyofayila leo katika Jengo la Michenzani Mall jijini Unguja.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika viwanja vya Michenzani Mall Jijini Zanzibar kufungua tawi la Benki ya CRDB na huduma za Islamic Banking

Rais wa Zanzibar Dk..ussein Ali Mwinyi amefungua Jengo la Maradhi ya akili.

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akifuatana na Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee,Jinsia na Watoto Mhe.Nassor Ahmed Mazrui (wa pili kushoto) na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa(wa pili kulia) pamoja Viongozi wengine mara baada ya kutembelea vyumba mbali mbali katika jengo la maradhi ya Akili lililojengwa kwa ufadhili wa Bw.Trond Mohn kupitia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland,Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mara baada ya kulifungua leo Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini Magharibi.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Maabara Nd. Mkubwa Ally (kushoto) fuatana na Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee,Jinsia na Watoto Mhe.Nassor Ahmed Mazrui (wa pili kushoto) wakati alipotembelea jengo la maradhi ya Akili lililojengwa kwa ufadhili wa Bw.Trond Mohn kupitia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland,Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mara baada ya kulifungua Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini Magharibi.
  • Rais wa Zanzibar na MBLM Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) akifungua pazia kuashiria Ufunguzi wa jengo la maradhi ya Akili Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini Magharibi lililojengwa kwa ufadhili wa Bw.Trond Mohn kupitia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland,Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa jengo la maradhi ya Akili lililojengwa kwa ufadhili wa Bw.Trond Mohn (kulia) akiwa na mkewe kupitia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland,Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar liliopo Kidongo Chekundu Wilaya ya Mjini Magharibi (katikati) Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee,Jinsia na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.

Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania.

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akimkaribisha Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Nabil Hajlaoui alipofika Ikulu jijini Zanzibar kujitambulisha leo akiwa na Mke wa Balozi Amna Hajlaoui.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(kulia) akizungumza na Mgeni wake Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Nabil Hajlaoui wakati wa mazungumzo yao alipofika Ikulu jijini Zanzibar kujitambulisha.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akimsikiliza Mgeni wake Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Nabil Hajlaoui wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Zanzibar alipofika kujitambulisha.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akiwa katika picha na Mgeni wake Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Nabil Hajlaoui mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Zanzibar alipofika kujitambulisha.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(kulia) akiagana na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Nabil Hajlaoui mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Zanzibar alipofika kujitambulisha.

Rais Wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amerejea nchini Tanzania leo baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa Mkutano wa Maonesho ya Biashara

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mwenyeji wake Kiongozi wa juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe.Mashego Dlamini, akikagua gwaride maalum aliloandaliwa wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Darban Afrika Kusini leo 16-11-2021, akirejea Nchini Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa ICC Darban
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudance Milanzi na (kushoto kwake) Kiongozi wa Juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe. Mashego Dlamini na ( kulia kwake) Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Edwin Lutageruka, wakati akiondoa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Darban Afrika Kusini akirejea Nchini Tanzani.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mwenyeji wake Kiongozi wa juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe.Mashego Dlamini, akikagua gwaride maalum aliloandaliwa wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Jijini Darban Afrika Kusini leo 16-11-2021, akirejea Nchini Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa ICC Darban
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na kuagana na Balozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini Mhe. Meja Jenerali (Mst) Gaudance Milanzi na Kiongozi wa Juu wa Serikali ya Afrika Kusini Mhe. Mashego Dlamini,alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Shaka Darban Jijini Afrika Kusini baada ya kumalizika kwa mkutano wa Ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa Nchi za Afrika uliofanyika katika ukumbi wa ICC Darban

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na kuzungumza na Wawekezaji Jijini Darban

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya El Sewedy kutoka Nchini Misri. Mhandisi.Ahmed El-Sewedy na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.Mhe.Omar Said Shaban na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania Mhe. Exaud Kigahe, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hotel ya “The 0yster Box “ Darban Nchini Afrika Kusini, baada ya ufunguzi wa Maonesho ya Biashara kwa wafanyabiashara wa Nchi za Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa ICC Jijini Darban Nchini Afrika Kusini.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Nchini Misri ukiongozwa na Kiongozi Mkuu ya Kampuni ya Elsewedy.Mhandisi Ahmed El Sewedy na (kulia kwa Rais) na(kushoto kwa Rais) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.Mhe Omar Said Shaban,mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya “The Oyster Box” Jijini Darban Afrika Kusini, baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Nchini Misri ukiongozwa na Kiongozi Mkuu ya Kampuni ya Elsewedy.Mhandisi Ahmed El Sewedy na (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais)Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar.Mhe Omar Said Shaban,mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya “The Oyster Box” Jijini Darban Afrika Kusini, baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Maonesho ya Wafanyabiashara wa Nchi za Afrika.