State House Blog

MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM TAIFA IKULU DAR.

  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akiendesha Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo,
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
  • Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam
  • Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungamo Mhe.Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Jamhuri nya Muungano Mhe.Job Ndugai,Spika wa baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid,
  • Wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar na MBLM Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Balozi Hussein Said Khatib kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Jaji Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Mabrouk Jabu Makame kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Rukia Mohammed Issa kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Juma Ali Juma kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Issa Mohammed Suleiman kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Ali Rajab Juma kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Joseph Abdalla Meza kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dkt,Idris Muslim Hija kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bibi Salama Mbarouk Khatibu kuwa Mkuu wa Wilaya yaMicheweni Pemba katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Kapteni Khatib Khamis Mwadini kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A.Unguja,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Rashid Hadid Rashid kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Abeid Juma Ali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Bakari Haji Bakari kuwa Katibu Mtendaji wa Bazara la Biashara la Zanzibar hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu .Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Wizara ya Fedha na Mipango
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Bw.Iddi Haji Makame kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango,hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar

Rais Dkt. Shein atembelea maonesho ya Sabasaba Dar es Salaam

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko zanzibar Balozi Amina Salum Ali(wa tatu kushoto) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Map
  • Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya Dar es Salaam Bw. Habibu Bukko wakati alipotembelea banda la VETA
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia biashara mbali mbali za vipodozi wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali na kulia mjasiria mali Fadhil Mohamed wa Kiembesamaki Zanzibar
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia biashara mbali mbali za vipodozi wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiangalia biashara mbali mbali za viatu vya Makubadhi na Mikoba wakati alipotembelea banda la vikundi vya Zanzibar, leo katika maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipangalia mashine ya kutengenea sabuni pamoja kuapata melezo kutoka kwa Mkurugenzi George M.Buchafwe wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam leo (kulia) mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Ziwanda vidogo vidogo (SIDO) Bw.Omar Jumanne Bakari
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Mkombozi Group (NGARABUTO) Bw.Amos Z.Mshina,kuhusu Usindikaji na Usambazaji wa Unga wa Muhugo katika maeneo ya Sengerema Mkoani Mwanza,wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa leo yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia biashara mbali mbali ya mikoba wakati alipotembelea leo maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba Jijjini Dar es Salaam,(kulia) Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa wote (EOTF) Mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa. Picha na Ikulu
  • Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akiuliza swali kwa mjasiliamali wakati alipotembelea banda la wanawake Wajasiliamali (WIPE),
  • Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kuhusiana na uzazi wa mpango, wakati alipotembelea banda la Wanawake na Maendeleo (WIPE),

Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini akutana na Rais Dkt. Shein.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea Mhe Song Geum-Young na kuzungumzia masuala mbalimbali ya uhusiano na ushirikiano.

Katika mazungumzo hayo Dk. Shein na balozi Young walisifu jitihada za serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Korea za kuimarisha uhusiano huo tangu nchi mbili hizo zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka ya tisini. “Tumefanya jitihada kubwa za kuimarisha uhusiano wetu na matokeo yake sasa nchi zetu zinashirikiana kwa karibu katika mambo mbalimbali katika nyanja za kidiplomasia, uchumi na maendeleo” Dk. Shein alimueleza Balozi huyo.

Alifafanua kuwa ushirikiano katika biashara na uwekezaji, elimu, afya na kilimo ambayo ni kati ya maeneo yaliyowekewa mkazo katika ushirikiano ni maeneo muhimu kwa kuwa yanasaidia jitihada za kupunguza kiwango cha umasikini hivyo kujenga ustawi wa wananchi. Dk. Shein alibainisha kuwa chini ya uhusiano huo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ikiwemo imekuwa ikifaidika na misaada mbalimbali ambayo imekuwa chachu katika kuongeza kasi ya jitihada za wananchi wa Tanzania kujiletea maendeleo.

Katika mazungumzo hayo Dk. Shein aliishukuru Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Korea kwa misaada yake kwa Serikali na watu wa Zanzibar na kuutaja mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji kuwa moja ya matokeo makubwa ya ushirikiamo kati ya nchi hiyo na Zanzibar. “Kupitia mradi huu wa umwagiliaji, tunatarajia kutimiza lengo letu la muda mrefu la kujitegemea kwa chakula hivyo ni habari njema kwetu kuwa taratibu za kuanza utekelezaji wa mradi huu zitakamilika hivi karibuni” Dk. Shein alieleza.

Pamoja na mradi wa kilimo cha umwagiliaji, Jamhuri ya Korea kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (KOICA) inaisaidia pia Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Ulimwenguni (FAO) mradi wa ufugaji wa samaki wenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 3.4. Dk. Shein alitambua mchango wa shirika la kazi za kijamii la Korea la SAEMAUL ambalo alisema limekuwa likifanya kazi nzuri za kusaidia maendeleo ya jamii katika maeneo ya vijijini hapa Zanzibar.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake inaupa kipaumbele uhusiano wake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ingependa kuona unaimarika siku hadi siku. Alifafanua kuwa ujumbe maalum wa nchi hiyo utakuja tena nchini mwezi Julai 2016 kwa mazungumzo zaidi ya ushirikiano baada ya mkutano kama huo wa ushirikiano uliofanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Balozi Young alieleza kufurahishwa kwake kuona zaidi ya vijana 80 wa kujitolea wa Kikorea wanashiriki hutoa huduma za kijamii katika sehemu mbalimbali za Tanzania ikiwemo Zanzibar. Alieleza kitendo hicho kuwa ni kilelezo kingine cha kuonesha na kuimarisha urafiki mzuri uliopo kati ya nchi yake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika mkutano huo Balozi Young alimhakikishia Dk. Shein kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo.

DKT SHEIN AKUTANA NA WAZIRI AUGUSTINO MAHIGA

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe,Augustino Mahiga alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]17/06/2016.