Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Mama Mariam Mwinyi, leo tarehe 03 Agosti 2026 amemtembelea na kumjulia hali msanii maarufu wa muziki nchini, Zuhura Othman Soud, maarufu kama Zuchu, kufuatia kujifungua mtoto wake na Naseeb Abdul almaarufu Diamond tarehe 01 Agosti 2026 katika Hospitali ya Saifee,  iliyopo Kata ya Kinondoni Mtaa wa Ada Estate, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mama Mariam Mwinyi amempongeza kwa kujifungua salama na kuwatakia kheri yeye pamoja na mtoto wao afya njema, maisha marefu yenye baraka na mafanikio.

Kwa upande wao,  Zuchu na Diamond wamemshukuru Mama Mariam Mwinyi kwa kutenga muda wa kufika kuwajulia hali na kuwatembelea wakieleza kuwa hatua hiyo ni faraja kubwa kwao na kwa familia katika kipindi hiki muhimu.