Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema hakuna neema kubwa zaidi ya Amani na kuwahimiza Waumini na Wananchi kuidumisha neema hiyo. ALhaji Dkt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 26 Disemba 2025 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa Kiembesamaki kwa Abdalla Rashidi, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alhaji Dkt, Mwinyi amewanasihi Waumini na Wananchi kwa Ujumla kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia Nchi Amani kama inavyoelekezwa katika Quraan. Aidha Dkt, Mwinyi amewakumbusha Waumini wa Dini ya Kiislamu kuongeza Ibada na Kumcha Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki muhimu cha Mwezi Rajabu .

Alhaji Rais Dkt Mwinyi ameendeleza Utaratibu wake wa Kujumiuika na Waumini wa Dini ya Kislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumma katika Misikiti mbalimbali hapa nchini.