Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 20 Februari 2024.Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itadumisha ushirikiano na mahusiano na benki ya CRDB.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum na Wakurugenzi mbalimbali wa Serikali kutoka Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.