Dk.Shein amekabithiwa Tunzo za Sinema zetu.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Tuzo ya Sinema Zetu na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume katika hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiangali CD za Michezo ya Wasanii wa Zanzibar zilizoshinda katika mashindano ya Tuzo ya Senima Zetu,Tanzania, baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibaer na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na kuwapongeza Wasanii wa Zanzibar kwa ushindi waliopata katika mashindano ya Sinema Zetu,walipofika Ikulu Zanzibar leo, kushoto kwa Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Nd.Salum Maulid wakiwa na Wasanii wa Filamu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar na Uongozi wa Wasanii wa Filamu Zanzibar waliosimama , waliokaa kulia kwa Rais Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume,Bi.Maryam Hamdani Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa Zanzibar na Bi. Khadija Ibrahim Dau (Bi.Hawa) Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu Zanzibar na kushoto Naibu Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Lulu Msham Abdalla, Mshauri wa Rais Masuala ya Sanaa na Utamaduni Mhe. Chimbeni Kheri na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Ndg Omar Hassan King.
Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid na Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge Justin Maturi (katikati) wakiongozwa na Mpambe Mwinyi Haji Abu(mwenye Siwa) wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiingia katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufungua Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) **Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai (kulia) Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge Justin Moturi (katikati) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid (wa pili kushoto) ** na Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Alitwala Kadaga wakisimama wakati Wimbo wa Taifa wa Ukipigwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi rasmi wa Mkutano huo unaofanyika Hotelini hapo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar uliofunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Afrika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Dk.Shein amezungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar ,wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo juzi mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar , kushoto kwa Rais Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kulia kwa Rais Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee
MSHAURI wa Rais Pemba Mhe.Dk. Maua Abeid Daftari akizingumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein. Hayupo pichani.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019,uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Bi. Khadija Khamis Rajab wa kwanza kushoto akisoma taarifa ya Utekelezaji Bajeti na Mpango Kazi ya Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2018, wakati wa mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali akiwasirisha mutasari wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, kulia Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na kushoto Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, hayupo pichani.
MKURUGENZI wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Ndg .Khatib Mwadin akijibu swali wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti ya Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) Dk. Said Seif Mzee
MKURUGENZI wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) Ndg .Khatib Mwadin akijibu swali wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti ya Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) Dk. Said Seif Mzee
BAADHI ya Watendaji wa Idara za Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa Wizara yao kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
Dk.Shein amekutana na Uongozi wa Wizara ya Afya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bi.Asha Ali Abdalla (katikati) alipokuwa akisoma wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Naibu Katibu Mkuu Bi.Halima Maulid Salum(kulia)
Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dk.Jamala Adam Taib (kulia) alipokuwa akichangia katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara hiyo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,Naibu Katibu Mkuu Bi.Halima Maulid Salum,(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bi.Asha Ali Abdalla
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Meneja wa Kitengo cha Maleria katika Wizara ya Afya Dk.Abdalla Suleiman Abdalla akitoa ufafanuzi kuhusu Maradhi ya maleria katika mkutano wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ulichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (katikati) alipokuwa akisoma muhtasari wa utekelezaji wa malengo ya mpango kazi kwa kipindi cha Julai 2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(kushoto) mshauri wa Waziri Dk.Mohamed Saleh Jidawi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee
Ufunguzi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali walioalikwa katika ufunguzi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar wakiwa katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli hiyo iliyopo Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati waliokaa) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Bw Rustamali Merani Shivji (wa pili kulia) wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo mara baada ufunguzi rasmi uliofanyika leo, Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini Magharibi,(kushoto) Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume na Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa (wa pili kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar uliofanyika leo, Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Mtendaji Mkuu wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Bw Rustamali Merani Shivji wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Hoteli hiyo mara baada ufunguzi rasmi uliofanyika leo, Mbweni Wilaya ya Magharibi (B).Mkoa wa Mjini Magharibi