Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi Ulinzi wa Uhakika siku ya Uchaguzi na kuwatka kujitokeza kwa wingi kutimiza hali yao ya Kidemokrasia. Dkt,Mwinyi amesema Serikali zote mbili zimejiandaa kuhakikisha kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura anapata fursa ya kutekeleza haki yake ya Msingi ya kikatiba ya kuchagua Viongozi.

Aidha Ameeleza kuwa Amani ,Muungano na Mshikamano ni Tunu za Taifa ambazo Chama cha Mapinduzi kimeahidi kuzitunza kwa maslahi ya Wananchi wote bila ya kujali asili ya Mtu au dini anayoabudu Rais,  Dkt Mwinyi amefahamisha kuwa Serikalli zote mbili zimeondoa aina zote za Ubaguzi ikiwemo Ubaguzi wa Dini na kwamba kitaendelea kudumisha Sera hiyo ili kutoa Uhuru wa Kuabudu kwa Waumini wa Imani zote.

Rais Dkt, Mwinyi ameushukuru Umoja wa Makanisa kwa kuandaa Maombi hayo aliyoyaelezea kuwa na Umuhimu mkubwa hususani wakati huu wa kampeni na kuelekea siku ya Uchaguzi.Rais Dkt Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 25 Oktoba 2025 alipozungumza katika Maombi ya Amani ya Kitaifa pamoja na kuuombea Uchaguzi Mkuu yalioandaliwa na Umoja wa Makanisa Zanzibar yaliofanyika Uwanja wa michezo wa Kizimbani Dole ,Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dkt, Mwinyi amesema Taasisi za kidini zina Wajibu mkubwa wa kuwaanda Waumini kuwa raia wema na kutoa mchango kwa Maendeleo ya nchi na kuahidi Serikali kuendelea kushirikiana na Taasisi hizo wakati wote.Mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi ameuhakikishia Umoja huo wa Makanisa Ushirikiano zaidi katika awamu ijayo endapo Wananchi watakipa ridhaa Chama Cha Mapinduzi kuiongoza tena Zanzibar kwa awamu nyengine na kuzipongeza Taasisi za kidini kwa misaada ya Kijamii inayotoa katika sekta ya Elimu ,Afya na Maji kwa Wananchi.

Rais Dkt, Mwinyi amewahkikishia Waumini wa Kikristo kuwq tayari kuzifanyia kazi Changmoto zote wanazokabiliana nazo hivi sasa na zitakazojitokeza baadae. Mwenyekiti na Mratibu wa Maombi hayo Askofu Dikson Kaganga amaeahidi kwa Umoja wa Makanisa Zanzibar kuendelea kuiombea nchi Amani,Umoja na Mshikamano ili lengo la kuwa na Amani ya Kudumu litimie pamoja na kuwataka kujitokeza kwa wingi Kupiga kura.