Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameyakaribisha Makampuni na Wawekezaji wa Uturuki kuwekeza Nchini hususan katika Maeneo ya Biashara ,Nishati na Miundombinu.Rais Dķt, ameyasema hayo leo tarehe 2 Mei 2026 alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa anayeshughulikia Masuala ya Afrika Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo Balozi Volkan Isikci akiamabatana na Balozi wa Uturuki Tanzania Balozi Bekir Geze waliofika Ikulu, Zanzibar.
Rais Dķt, Mwinyi Vikao vya aina hiyo vinaimarisha Uhusiano wa muda mrefu baina ya Nchi hizo mbili na kutoa fursa mpya ya kubainisha Maeneo mapya ya Ushirikiano hususani katika Masuala ya Biashara na Uwekezaji na kueleza kuwa ni wakati sahihi kwa Wawekezaji wa Uturuki kuja kuwekeza katika Miradi ya Madini,Kilimo ,Utalii, Afya na Miundombinu.
Dkt,Mwinyi ameeleza kuwa kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikinunua Chuma kutoka Uturuki hivyo ni vema kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara waNchi hiyo kuwekeza Tanzania na kuzongezea Thamani bidhaa zinazozalishwa Nchini ikiwemo Korosho, Chai na Kahawa ambazo zimekuwa zikiuzwa kama Malighafi.
Amesema Zanzibar inafanya juhudi kubwa za kuwa na Umeme wa Kujitegemea na eneo hilo lina fursa kubwa ya Uwekezaji hivyo ni Vema Wawekezaji wa Uturuki wakatumia fursa hiyo pamoja na eneo la Uimarishaji wa Viwanja wa Ndege kuja kuwekeza. Aidha Rais Dķt, Mwinyi amesifu Misaada inayotolewa na Nchi hiyo kwa Tanzania ikiwemo Zanzibar katika sekta za Elimu ,Afya ,Kilimo na Miundombinu na Fursa za Mafunzo Nchini humo na kusisitiza kuongezwa zaidi .
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Uturki,Balozi wa Nchi hiyo aliyepo Tanzania Balozi Bekir Geze amesema Mataifa hayo ni rafiki na kueleza kuwa ni wakati wa kufungua Ukurasa mpya wa Ushirikiano na kufanya kazi pamoja hususani katika Eneo la Biashara na Uwekezaji.
Naye Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Afrika Balozi Volkan Isikci ameihakikishia Tanzania ikiwemo Zanzibar Ushirikiano zaidi kupitia Mkakati wa Nchi hiyo kwa Maendeleo ya Nchi za Afrika kuhakikisha Maendeleo ya Kiuchumi na Ustawi wa Wananchi katka nyanja Mbalimbali ikiwemo Elimu,Afya ,Kilimo ,Miundombinu na Utalii.
.jpeg)