Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM Zanzibar, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amerejesha fomu za uteuzi katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Maisara,  Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 6 Septemba 2025 akiwa mgombea wa kwanza kufanya hivyo.

Dkt. Mwinyi amewashukuru wanachama wa CCM kwa kumdhamini na kuwataka wagombea wenzake kuhubiri amani wakati wa kampeni.Mwenyekiti wa ZEC, Jaji George Joseph Kazi, amesema hatua inayofuata ni uhakiki na zoezi la pingamizi kabla ya kutangaza majina ya wagombea rasmi.

Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar zitaanza 13 Septemba, uchaguzi wenyewe utafanyika tarehe 29 Oktoba 2025.