Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Burundi kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 60 ya nchi hiyo zinazotarajiwa kufanyika kesho Julai 01,2022.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi aliagwa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah.
Rais Dk. Mwinyi ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, katika safari yake hiyo amefuatana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo mkewe Mama Mariam Mwinyi.