1. MAJAJI WA MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 94(2) cha Katibaya Zanzibar ya 1984,Raiswa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa
Dkt. Ali Mohamed Shein amewateua Bwana Khamis Ramadhan Abdalla na Bibi Aziza Iddi Suweid kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

2. KATIBU WA TUME YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chin iya Sheria ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Namba 4 ya 2015, kama ilivyorekebishwa na Sheria Namba 4 ya 2017, Kifungu cha 10(a)(1), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe shimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibuwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


3. NAIBU KATIBU MKUU KATIKA OFISI YA RAIS, KATIBA, SHERIA, UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 50(4) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungucha 12 (1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya Namba 2 ya 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana George Joseph Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora anaeshughulikia masuala ya Katiba na Sheria.

4. NAIBU MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA BANDARI

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya 1997, Raiswa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Kapteni Juma Haji Juma kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.

Uteuzi wote huo umeanza tarehe 29 Septemba 2017.

Viongozi wa lioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, Katibu waTume ya Maadili ya Viongozi na Naibu Makatibu Wakuu wa natakiwa kuripoti Ikulu siku ya Jumatatu tarehe 2 Oktoba 2017saa 3:30 Asubuhi tayari kwa kuapishwa.