Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

1. OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS

i. Bwana Abdulla Hassan Mitawi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais.

2. WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

i. Bibi Saum Ali Said ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

ii. Bwana Joseph John Kilangi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Uteuzi huo umeanza leo tarehe 12 Machi, 2018.