State House Blog

Rais wa Zanzibar amehudhuria hafla ya kuapishwa Rais wa Tanzania Ikulu Dar Es Salaam

  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride maalum la JWTZ baada ya kupokea Salamu ya heshima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam
  • RAIS Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam leo 19-3-2021 na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi,Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.Job Ndugai , Jaji Mkuu wa Tanzania MheProf. Ibrahim Hamis Juma na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Bashiru Ally
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Spika Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Prof Ibrahim Hamis Juma, baada ya kumaliza kuzungumza na Viongozi na wageni waalikwa baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  • MARAIS Wastaaf na Wageni waalikwa wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wananchi baada ya kuapishwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam