State House Blog

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amelihutubia Bunge Jijini Dodoma

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika paredi ikiongozwa na Mhe Hassan Zungu wakielekea katika ukumbi wa Bunge wakati wa hafla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulihutubia Bunge leo 22-4-2021 Jijini Dodoma.
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia hutuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma na (kulia kwake) Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere na Mke wa Rais Mstaaf wa Tanzania Awamu ya Pili Mhe Ali Hassan, Mama Siti Mwinyi na (kushoto kwake)Mke wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mama , wakimsikiliza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akilihutubia Bunge Jijini Dodoma.
  • RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiingia katika ukumbi wa Bunge kwa paredi kwa ajili ya kulihutubia Bunge leo 22-4-2021 Jijini Dodoma
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akiingia katika ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kulihutubia Bunge na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Prof Philip Isdor Mpango na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Tulia
  • VIONGOZI Wakuu Wastaaf wakifuatilia hutuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Bunge Jijini Dodoma.
  • RAIS Mstaaf wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa na Marais Wastaaf wakielekea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Jijini Dodoma.wakati wa hafla ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kulihutubia Bunge.