State House Blog

Rais wa Zanzibar Alhajj Dk.Hussein Mwinyi amejumuika na Viongozi na Wananchi katika Maziko ya Hayati Rais Mstaafu wa Tanzakia awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi Mangapwani Zanzibar.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi mbalimbali baada ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza ya Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi , iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar leo 2-3-2024.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi mbalimbali baada ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza ya Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi , iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar leo 2-3-2024.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi mbalimbali na Wananchi katika Sala ya jeneza ya kumsalia Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi , iliyoongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi
  • VIONGOZI Wastaafu wakitowa heshima za mwisho kwa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi , wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar leo 2-3-2024
  • VIONGOZI wa Dini Zanzibar wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar kwa ajili ya Sala ya Jeneza iliyofanyika katika Masjid hiyo leo 2-3-2024
  • WAJANE wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi Mama Khadija Mwinyi na (kulia ) Mama Siti Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kwa ajili ya kuagwa na kutowa heshima za mwisho kwa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan, hafla hiyo iliyofanyika leo 2-3-2024.
  • RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mweyekiti wa Baraza la Mapinduzi . Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi wakitowa heshima za mwisho kwa Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya New Amaan Complex Amaan Zanzibar leo 2-3-2024
  • GARI Maalum la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa limebeba Mwili wa Hayati Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhajj Ali Hassan Mwinyi likipita katika barabara ya Amani kuelekea katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kwa ajili ya kutowa heshima za mwisho kwa Viongozi wa Kitaifa na Wananchi wa Zanzibar