State House Blog

Rais wa Zanzibar Alhajj Dk.Hussein Mwinyi amelihutubia Baraza la Eid El Fitry ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar 22-4-2023.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Amani Karume na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein, baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika 23-4-2023 katika ukumbi wa Sheikh. Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
  • RAIS Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akiwasalimia Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakati akiondoka katika ukumbi wa Sheikh.Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry, lililofanyika 22-4-2023 katika ukumbi huo na kuhutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi.
  • VIONGOZI na Wageni waalikwa wakijumuika katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibarb 22-4-2023.
  • MABALOZI Wadogo wanaofanyia Kazi zao Zanzibar wakijumuika katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Fitry lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na kuhutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi 22-4-2023
  • BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakijumuika katika kutikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa hutuba ya Baraza la Eid El Fitry, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh. Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar lililohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, 22-4-2023
  • VIONGOZI wa Serikali na Marais Wastaafu wa Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid El Fitry, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akilihutubia katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja leo 22-4-2023, baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika katika kutikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa hutuba ya Baraza la Eid El Fitry lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 22-4-2023, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na (kushoto kwa Mufti) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman
  • MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwatunza Wasomaji wa Qaswida Maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid El Fitry, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh.Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar 22-4-2023