State House Blog

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk Hussein Ali Mwinyi amehudhuria Misa na Ibada Maalum ya kuwaombea Viongozi wa Kitaifa.

  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiikristo Chato na Viongozi mbali mbali wa Serikali baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada Maalum ya kuwaombea Viongozi mbali mbali,iliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria Chato Mkoa wa Geita, iliongozwa na Baba Askofu Muhashamu Seveline Niwemgizi.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakifuatilia Misa na Ibada Maalum ya kuwaombea Viongozi wa Kitaifa iliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria Chato, iliongozwa na Baba Askofu Mhashamu Seveline Niwemgizi
  • BABA Askofu Muhashamu wa Jimbo Katoliki Ngara Seveline Niwemgizi (katikati) akiwa na baadhi ya Maaskofu wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiikristo Geita baada ya kumalizika kwa Ibada na Misa Maalum ya kuwaombea Viongozi iliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria Chato Mkoa wa Geita.
  • BABA Askofu Muhashamu wa Jimbo Katoliki la Ngara Askofu Seveline Niwemgizi akiongoza Misa na Ibada Maalum ya kuwaombea Viongozi iliofanyika katika Kanisi la Mtakatifu Bikira Maria Chato.
  • MJANE wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Mama Maria Nyerere akishiriki katika Misa na Ibada Maalum ya kuwaombea Viongozi wa Kitaifa iliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria Chato.
  • WAUMINI wa Dini ya Kikiristo Mkoani Geita wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada maalum ya kuwaombea Viongozi iliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria Chato Mkoa wa Geita.
  • RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiikristo Chato na Viongozi mbalimbali wa Serikali baada ya kumalizika kwa Misa na Ibada Maalum ya kuwaombea Viongozi mbali mbali,iliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria Chato Mkoa wa Geita, iliongozwa na Baba Askofu Muhashamu Seveline Niwemgizi.