Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amerejea nchini leo akitokea Burundi ambapo alihudhuria sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa nchi hiyo.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi alipokewa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah.

Rais Dk. Mwinyi ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika safari yake hiyo alifuatana na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo mkewe Mama Mariam Mwinyi.