MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za Makao Makuu ya CCM maarufu White House Jijini Dodoma, ambacho kilihudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya (CCM). Dk. Hussein Ali Mwinyi.