1. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 50(4) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu(Uwezeshaji) katika Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto.

2. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 13(2)(a) cha Sheria ya Shirika la Biashara la Taifa la Zanzibar(ZSTC) Namba 11 ya 2011, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua tena Bwana Kassim Maalim Suleiman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya ZSTC katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko.

3. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungu 15(1) cha Sheria ya Tawala za Mikoa Namba 8 ya 2014, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Yussuf Mohammed Ali kuwa KATIBU TAWALA WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.

4. Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 53 cha Katiba ya Zanzibar ya 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Bwana Juma Nyasa Juma kuwa Afisa Mdhamini-Pemba katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.
Uteuzi huo umeanza tarehe 09 Februari, 2016.