Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Ali Moh’d Shein, aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na wakulima wa bonde la mpunga la Ukele mara baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Tuta la kuzuia maji ya chumvi kuigia katika bonde la mpunga na kueleza kuwa hali hiyo ilikuwa inamsikitisha sana na Serikali anayoiongoza ikaona haja ya kuwasaidia iliwaondokane na tatizo hilo.Dk. Shein akiwa katika ziara yake anayoifanya ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba ya kuangalia Shughuli mbali mbali za maendeleo aliendelea kusema kuwa Kilimo kinaweza kuwakombowa Wananchi na kuahidi serikali itaendelea kuwaunga mkono.Alisema kuwa Serikali imesikia Kilio cha Wakulima na itahakikisha kuwa inarahisisha matatizo ya Wananchi ikiwemo kuwapatia mbinu mbali mbali za Kilimo kwa kuwapatia Pembejeo na Wataalamu wa Kilimo.Hata hivyo, Rais wa Zanzibar, aliwataka Wakulima na Wananchi kwa Ujumla kuhifadhi Mazingira kwa kupanda miti ikiwemo Mikandaa na kuilinda na wasiwaruhusu watu wengine kuikata kwani moja ya sababu ya kuingia maji katika Mashamba yao ni kukata Miti katika eneo hilo.