Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee walishiriki.
Akisoma Taarifa ya utangulizi ya utekelezaji wa Malengo makuu hayo ya Wizara, Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Ali Juma Shamuhuna alisema kuwa hata hivyo, idadi ya wanafunzi walioandikishwa kujiunga na chuo hicho imeongezeka kutokana wanafunzi 1,413 hadi wanafunzi 1,837.Alisema kuwa ongezeko hilo la wanafunzi limetokana na uamuzi wa SUZA kuongeza program mbili mpya za masomo.Aidha,Uongozi huo ulieleza kuwa idadi ya wanafunzi wanaosoma katika taasisi za Elimu ya Juu wanaodhaminiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzibar imeongezeka sana kutoka wanafunzi wapya 209 hadi wanafunzi wapya 800.Uongozi huo ulieleza kuwa ongezeko hilo limetokana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuongeza bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Zanzibar kutoka TShs. Bilioni 4 hadi TShs. 8.
Wizara hiyo pia, ilieleza kuwa ujenzi wa skuli 13 mpya za sekondari kati ya 16 umekamilika ambapo skuli 9 mpya zimeshaanza kuchukua wanafunzi na wakati huo huo ujenzi wa skuli tano mpya za sekondari za ghorofa unaendelea katika maeneo ya Mpendae, KiembeSamaki na Kwamtipura, Mkoa wa Mjini Magharibi, Kibuteni kwa upande wa Mkoa wa Kusini Unguja na Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba.Wizara ilieleza kuwa, awamu ya kwanza ya ujenzi wa kampasi ya Chuo cha Ualimu cha Benjamin William Mkapa huko Mchanga Mdogo, Pemba umekamilika na ujenzi wa awamu ya pili unaendelea na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili mwaka 2013.